Serikali imetoa tamko lake kwa mara ya kwanza tangu litokee tukio la mwalimu wa shule ya msingi ya Kibeta iliyopo Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera kumchapa fimbo mwanafunzi wa darasa la 5 aliyejulikana kwa jina la Sperius Eradius (13) kwa tuhuma za kuibiwa mkoba.
Serikali kupitia Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako akiongea na Waandishi wa Habari leo Jumatano Agosti 29, 2018, amesema kuwa tukio hilo lilikuwa ni la bahati mbaya na tayari hatua za kisheria zimechukuliwa.

